Mwandishi David Cannadine anajenga hoja kuwa dhamira ya utawala wa Himaya ya Uingereza duniani ilikuwa ni kuusambaza ustaarabu wa mfumo wa maisha ya Kiingereza kwenye mataifa mengine na sio kuyadunisha wala kuyadharau mataifa hayo. Ismail Jussa anaichambua nadharia hii na uwiano wake na uhalisia wa utawala wa Muingereza visiwani Zanzibar.