Our writings do not only define what we are and how we perceive the world around us but they also are an image of ourselves that will remain many years after we have departed this world.

Mohammed Ghassani

“Tangu hapo nikagundua kuwa nimekutana na mshairi chipukizi gwiji, mwenye kipawa kikubwa chenye mwangwi wa kazi za washairi maarufu wa Kiswahili. Kazi za akina Muyaka bin Haji Al-Ghassany, Abdilatif Abdalla,  Ahmad Nassir wa Mvita, na akina Kamange na Sarahani wa Pemba.” – Kwenye Machozi Yamenishiya: Diwani ya Mohammed Ghassani

Profesa Said A. M. Khamis

“Nimemjua Mohammed Ghassani kwa zaidi ya miaka kumi kupitia maandishi yake mbalimbali yanayochapishwa kwenye magazeti ya Kiswahili nchini Tanzania…. Kwa hakika, nilivutiwa sana kwa umahiri uliomo kwenye maandishi yake, kwa ufundi wake wa lugha katika kuwasilisha mawazo yake na kwa uzito wa hoja zake.” Kalamu ya Mapinduzi: Mapambano Yanaendelea

Profesa Ibrahim Noor