Leo nimepata ujumbe mfupi kutoka kwa mwanafunzi mwenzangu wa zamani. Ameniuliza: hivi wewe Mohamed huko wapi siku hizi?
Nikamjibu: unakusudia niko au siko wapi? Kama niko wapi, basi niko Ujerumani na kama siko wapi, basi siko kwengine kote kusikokuwa Ujerumani.
Matumizi ya herufi ‘h’ yanawapa tabu sana baadhi ya watumiaji wa Kiswahili, ambao hii si lugha yao ya kwanza au hata ya pili.
Mwengine aliniandikia ‘Nashaadia Mungu wa aki ni mmoja tu’, akimaanisha anashahadia Mungu wa haki. Mahala pa kuiweka ‘h’ wanaiondoa na mahala inapoanzia voweli ya a, u, e, o au i wanaitanguliza h.
Kiswahili kina wenyewe.