Ndugu zangu na jirani, sikizeni nawambia
Washamba na wa mjini, wa mbali niagizia
Simuogopi fulani, kula mtu asikia
Muungano siutaki, miye sina haja nao
Hata uwe maarufu, na watu wauwanie
Usiwe na khitilafu, Mola auondolee
Sitaki ushanikifu, atake autakae
Muungano siutaki, miye sina haja nao
Tulikuwa na rafiki, twenda tukirudi nae
Ya furaha na ya dhiki, yote tulimpaye
Akajifanya kisiki, makusudi tumkwae
Muungano siutaki, tena sina haja nao
Seyph Njugu
26 Aprili 2011
Zanzibar