“Tangu hapo nikagundua kuwa nimekutana na mshairi chipukizi gwiji, mwenye kipawa kikubwa chenye mwangwi wa kazi za washairi maarufu wa Kiswahili. Kazi za akina Muyaka bin Haji Al-Ghassany, Abdilatif Abdalla, Ahmad Nassir wa Mvita, na akina Kamange na Sarahani wa Pemba.” – Kwenye Machozi Yamenishiya: Diwani ya Mohammed Ghassani