Ahmed Rajab

Tukiviacha vitambulisho vya isimu zake, Mohammed Ghassani ana vipaji vinavyomfanya awe na vitambulisho vingine tafauti: mshairi, mtangazaji wa redio ya kimataifa, mwanahabari, mwandishi, mpiga picha, mchapishaji vitabu na gwiji wa mitandao ya kijamii. Kwa ufupi, na kwa hakika, yeye ni taasisi kamili. Ni taasisi ya mtu mmoja yenye kukhusika na tasnia ya mawasiliano, kwa upana wake wote.