Continue reading “Ninaishi Magharibi”Kwa lugha na utamaduni wangu, magharibi ina maana nyingi: ndiko jua linakotulia likaibadilisha leo kuwa jana na kuitayarisha kesho kuwa leo. Ndicho kielelezo pia cha kumalizika kwa maisha ya mwanaadamu ya hapa duniani, maana magharibi kawaida huja na giza, na giza ni alama ya mauti. Magharibi pia ni nadharia ya kisiasa kwenye medani za kilimwengu na lugha yangu imeipokea hivyo hivyo – kuwa ni mataifa ya Ulaya na Marekani yanayoambiwa yameendelea kiuchumi, kisiasa na kijamii.