Nimekua nikitafakari matamshi ya hivi juzi tu na hotuba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jakaya Khalfani Mrisho Kikwete mkoani Singida alipokuwa akizungumza kwa kiburi na kusema uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa na dosari kubwa na baada ya kuzungumza na wenzake wakakubaliana na maamuzi ya Tume ya Uchaguzi (ZEC) kuwa eti uchaguzi urejewe. Nilitikisa kichwa na kucheka. Nikicheka kwa sababu nikijiuliza hivi kweli katika dunia hii ya leo, kiongozi anaweza kujidanganya, kuudanganya umma na jumuiya ya kimataifa na kuamini kwamba matamshi yake yamepokewa kuwa ni sahihi?
Continue reading “Kikwete azungumza asichokiamini akitutaka tumuamini”