Wakati Zanzibar inapata uhuru wake uliodumu kwa mwezi mmoja kabla ya kupinduliwa na kisha kuunganishwa na Tanganyika kulikoifanya iwe sehemu ya dola la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanadiplomasia wa Kimarekani, Don Petterson, alikuwa kwenye mwanzoni mwa kazi zake za kibalozi nchini Zanzibar. Kupitia kurasa za kitabu hiki, anazungumza alichokishuhudia na alivyokifahamu kwa mtazamo wa Kimarekani.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Revolution in Zanzibar cha Don Petterson”Tag: Tufunuwe Kitabu
TUFUNUWE KITABU: Gone With the Tide cha Fatma Jinja
Bi Fatma Jinja aliyaishi maisha yake akipitia milima na mabonde na sehemu kubwa ya namna alivyokabiliana nayo haikuwahi kufahamika na waliokuwa kando yake ambao, badala yake, waliyatafsiri makabiliano hayo kwa wapendavyo wenyewe. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za moja kati ya vitabu vyake vitano, Gone With the Tide, kinachosimulia hadithi ya maisha yake.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Gone With the Tide cha Fatma Jinja”TUFUNUWE KITABU: Zanzibar: The Last Years of the Protectorate
Leo, ismail Jussa anachambuwa jinsi Bwana Maulid Mshangama kupitia kitabu chake “Zanzibar: The Last Years of the Protectorate” anavyotowa ushahidi wa kina wa namna utawala wa Waingereza ulivyopanga vitimbi na hila za makusudi dhidi ya Zanzibar kuhakikisha kuwa visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi kamwe havisimami kama taifa huru linalojitegemea.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Zanzibar: The Last Years of the Protectorate”TUFUNUWE KITABU: Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha
Sheikh Thabit Kombo Jecha ni miongoni mwa wazee wa Kizanzibari walioshiriki kikamilifu katika siasa za kabla na baada ya uhuru na mapinduzi visiwani Zanzibar akishikilia nafasi mbalimbali ndani ya chama cha Afro-Shiraz Party na baadaye CCM na pia kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ismail Jussa anatupitisha leo kwenye kurasa za simulizi za Sheikh Thabit kwa mujibu wa zilivyoandikwa na Kanali Hosana Mdundo wa Jeshi la Wananchi la Tanzania.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha”