UCHAMBUZI

TUFUNUWE KITABU: Mafunzo kutoka The Asian Aspiration

Kitabu cha The Asian Aspiration kilizinduliwa mwishoni mwa mwezi Julai 2021 visiwani Zanzibar, na miongoni mwa wageni 50 waliohudhuria kwenye uzinduzi huo ni Ismail Jussa, ambaye kwenye Silsila hii ya kwanza anatudondolea baadhi ya mafunzo ambayo Zanzibar inaweza kujifunza kutoka mataifa ya Asia kuelekea maendeleo na ustawi wa watu wake.