PODCAST

Miye Zombi/I am a Zombie

Mama aliponizaa, alidhani kazaa mtu
Akanilea nikuwe
Akanifunza ili niwe
Binaadamu si jiwe
Bali mara akazuka –
Nduli akaja nitwaa!

When my mother gave birth to me
She thought she’d brough a human being
To this challenging world
She brought me up
And taught me how to behave
As a human being and not an animal
But then came a monster and took me away!PODCAST

Kati ya Pendo na Chuki/The Line Between Love and Hate

Kati ya pendo na chuki, pana mpaka mwembamba
Hata pima haufiki, ukiupima kwa kamba
Jana ulomuashiki, nyimboni ukamuimba
Leo bure humtaki, akitajwa unavimba

A line between love and hate is but so thin
Not even a yard if measured with thread
The one whom you yesterday desired –
For whom you sang all songs
Today, they are just rubbish 
And good for nothing

PODCAST

Dunia ni Ndogo/So Small is This World

Dunia ni ndogo, haitoshi kuficha siriyo
Tafuta pengine, kama napo, watu ‘siwe nayo
Kwa dunia hii, ni bilashi kuyasiri hayo
‘Kisema ni uzushi, ‘taoneshwa yale yaliyo
Dunia ya mtandao!

So small is this world to hide your actions
Search for somewhere else if ever be
For this world nothing you could hide
And when you deny, you’d be shown all that were
The world of networks!

PODCAST

Mbona?/Why a U-Turn?

Mbona wesema husemi, na hivi umo wasema, kipi kikusemacho?
Ulisema husimami, kwako ni mbele daima, kipi kikurejeshacho?
Wesema husemi nami, tena kwa kunamba koma, leo kipi kikupacho?

You said you wouldn’t say anything
Yet now you do
What makes you do so?
You said you wouldn’t stop
Forward you would go
What makes turn back?
You said you wouldn’t speak to me
You even told me to behave
Why has now today prompted you –
Why are taking a U-Turn?

Soundtrack: Ally F. Juma