Mauti ewe mauti, ukija kama hujaja
Huwa waja katikati, ya maisha yetu waja
Katikati ya wakati, na kati ya zetu haja
Na hata tukikutaja, wewe khabari hupati
Nimepokea habari ya Kaka yangu, Mzee wangu, Muhisani wangu, Sheikh Sulaiman Al Shukaili, kuitikia wito wa Aitaye akalazimika kuitikwa. Asubuhi hii karudi kwa Mola wake. Allah Ampokee ilhali keshamsamehe makosa yake na aifanye pepo iwe nyumba yake. Amin Yaa Rabb. Continue reading “Taazia: Kwaheri Maalim Suleiman Shkeli wa Pandani”