KISWAHILI KINA WENYEWE

Ni “kiasi cha…” sio “kiasi ya…”

AbdilatifKwa uchache wa nifahamuvyo, lugha fasaha ni kusema “kiasi cha…”, basi haidhuru iwe ni kwa watu au kwa vitu. Yaani, kiasi cha watu kumi, au kiasi cha miti kumi. Kama  ambavyo twasema, kitabu cha…, kisa cha…, kiatu cha…, kitambo cha…, na kadhalika, wala hatusemi kitabu ya…, kisa ya…, kiatu ya…, wala kitambo ya… Na ni hivyo kwa sababu maneno yote hayo yamo katika ngeli ya KI/VI. Basi ikiwa kwa maneno hayo niliyoyatolea mfano hatuyatumilii “ya”, kwa nini iwe kwa neno “kiasi”?

Continue reading “Ni “kiasi cha…” sio “kiasi ya…””

KISWAHILI KINA WENYEWE

Kitenzi ‘piga’ na ladha yake

Kiswahili kina ladha yake. Hapana shaka ni lugha zote, ingawa kwetu hili ndilo titi la mama, halishi hamu. Kitenzi ‘piga’ kinaweza kuonekana kuwa na maana mbaya katika hali yake ya awali, maana humaanisha ‘shambulia’, ‘dhuru’, ‘umiza’ na mengine yenye mshindo kama huo. Continue reading “Kitenzi ‘piga’ na ladha yake”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Herufi na Sauti za Kiswahili

Kiswahili kilipoanza kurikodiwa kimaandishi hakikuwa kikiandikwa kwa herufi hizi zinazoitwa za Kilatini, bali kwa zile za Kiarabu. Kwa mtazamo wangu, miongoni mwa misiba mikuu iliyokikumba Kiswahili ni huu wa kubadilishwa herufi zake mwanzoni mwa karne ya 19 baada ya upwa wa Afrika Mashariki kuvamiwa na Wazungu wakoloni. Continue reading “Herufi na Sauti za Kiswahili”