BLOG POSTS, KISWAHILI KINA WENYEWE

SIMULIZI ZA BI TIME: Hadithi za Ncha Saba

JAMII za Waswahili daima zimekuwa na mihimili inayoshikilia silka na tamaduni zake. Zimekuwa na taasisi imara za ujenzi na uendelezaji wa maisha, mitazamo, falsafa na imani zao. Kuanzia chini kabisa hadi juu kabisa, maisha ya watu wa Uswahilini huwa si matupu. Kila ombwe hujazwa kwa tanzu, bahari na mikondo ya sanaa na usanii, fasihi na ufasaha.

Continue reading “SIMULIZI ZA BI TIME: Hadithi za Ncha Saba”
UCHAMBUZI

Taazia: Kwaheri Maalim Suleiman Shkeli wa Pandani

Mauti ewe mauti, ukija kama hujaja
Huwa waja katikati, ya maisha yetu waja
Katikati ya wakati, na kati ya zetu haja
Na hata tukikutaja, wewe khabari hupati

Nimepokea habari ya Kaka yangu, Mzee wangu, Muhisani wangu, Sheikh Sulaiman Al Shukaili, kuitikia wito wa Aitaye akalazimika kuitikwa. Asubuhi hii karudi kwa Mola wake. Allah Ampokee ilhali keshamsamehe makosa yake na aifanye pepo iwe nyumba yake. Amin Yaa Rabb. Continue reading “Taazia: Kwaheri Maalim Suleiman Shkeli wa Pandani”