BLOG POSTS

LULU ZA ZANZIBAR: Kanali Ali Mahfoudh, kamanda wa ukombozi mashariki na kusini ya Afrika

Bi Naila Majid Jidawi mwenye umri wa miaka 77, anasimulia kuhusu mumewe, Marehemu Kanali Ali Mahfoudh, aliyezaliwa na kukulia Zanzibar, akapata mafunzo ya kijeshi Cuba na akawa miongoni mwa walioshiriki kuipindua serikali ya uhuru ya Zanzibar mwaka 1964, lakini akafungwa miaka kumi jela kwa tuhuma za mauaji ya Mzee Abeid Karume na akachukuliwa na Rais Samora Machel wa Msumbiji akiwa mshauri mkuu wa masuala ya ulinzi na vita vya ukombozi mashariki na kusini mwa Afrika.