UCHAMBUZI

Zanzibar ijifunze maana ya mapinduzi kutoka Oman

Kwa makusudi kabisa, wenye satwa ya kutunga sera na mwelekeo wa taifa letu wanataka ionekane kama kwamba uhusiano kati ya Zanzibar na Oman ulianza mwaka 1832 pale Sayyid Said bin Sultan Al-Busaid alipoanzisha utawala wake kisiwani Unguja na kisha kuhamishia rasmi makao yake makuu kutoka Maskat na kuyaleta kisiwani hapo miaka minane baadaye. Wakirudi nyuma zaidi, watakutajia 1698 baada ya kumalizika Vita vya Wareno. Continue reading “Zanzibar ijifunze maana ya mapinduzi kutoka Oman”

UCHAMBUZI

CCM Z’bar haina uhalali kujinasibisha na Mapinduzi

Ukizingatia hotuba za Marehemu Mzee Abeid Karume na matendo yake wakati wa uhai wake, ukazingatia marudio ya kauli za Marehemu Karume kupitia kwa mjane wake, Mama Fatma Karume, ukasikiliza hotuba moja tu ya Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha aliyoitoa katika moja ya mikutano yake na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), moja kwa moja unapata maana na malengo halisi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya tarehe 12 Januari 1964 na kisha unahitimisha kuwa mshirika mkuu kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, yaani CCM, yuko mbali kabisa na malengo ya Mapinduzi hayo na, hivyo, amepoteza kabisa uhalali wa kujinasibisha nayo.

Continue reading “CCM Z’bar haina uhalali kujinasibisha na Mapinduzi”