KISWAHILI KINA WENYEWE

N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini

Siku ilikuwa Jumatano. Tarehe ilikuwa 1 Septemba 2010. Majira yalikuwa ya saa 4:00 usiku. Mahala palikuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakumbuka kila kitu kuhusu siku hiyo. Nikiwa kwenye sehemu ya kusafiria abiria waitwao wa kimataifa, nilitoa simu yangu ya mkononi nikawasiliana na watu kadhaa kwa nia ya kuwaaga. Kati yao ni mama zangu wawili, aliyenizaa Abeida bint Nassor na aliyenilea Salama bint Said, mke wangu Tauhida bint Mkwale na dada yangu Fatma bint Khelef. Continue reading “N’na Kwetu: Sauti ya Mgeni Ugenini”