BLOG POSTS

A Chat with a Swahili young poet Bashiru Abdallah

Reading his verses and stanzas written in pure coastal Swahili, one can hardly notice that Bashiru Abdallah was born and raised far away from the sea shores of Tanzania. His mastery of the language is mind-blowing.

KISWAHILI KINA WENYEWE

Kurasa Mpya: Fungamano la Malenga

Ushairi unatambuliwa kuwa miongoni mwa sanaa kongwe kabisa kwa mwanaadamu. Jamii yoyote inayojitambuwa kwa ukale na ukongwe wake, basi utaikuta ndani yake ikiwa na sanaa ya ushairi kama moja ya dalili za uwepo wake wa zama na zama. Haitoshi hayo, ushairi pia unachukuliwa na wasomi wa taaluma za kibinaadamu, kuwa moja ya nguzo kuu za ilimu ya falsafa. Kwa ujumla, fasihi – ambayo yenyewe ndiyo mama wa maarifa ya mwanaadamu – inabebwa na tanzu nyingi, na kongwe yao ni ushairi. Continue reading “Kurasa Mpya: Fungamano la Malenga”