Kumekuwa na mjadala mrefu miongoni mwa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ikiwa kile kichachoitwa Kiswahili Sanifu ni lugha kamili na tafauti na lugha nyengine zinazozungumzwa kwenye maeneo yanayopakana nacho, kama vile Kimakunduchi (au Kikaye) kinachozungumzwa kusini mwa kisiwa cha Unguja, au zote kwa pamoja ni lahaja za lugha moja kuu, yaani Kiswahili. Msikilize Dk. Hans Mussa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichambua tafauti baina ya Kimakunduchi na Kiswahili Sanifu mbele ya hadhara ya Kongamano la 29 la Kiswahili la Bayreuth, kusini mwa Ujerumani. Continue reading “Uhusiano baina ya Kimakunduchi na Kiswahili Sanifu”
Tag: Kongamano la Kiswahili
Sitiari katika kazi za fasihi
Wataalamu na wachambuzi wa fasihi wanakipa umuhimu mkubwa kipengele cha sitiari (uhamishaji wa sifa kutoka kitu kimoja kwenda chengine) miongoni mwa tamathali za semi katika fasihi. Kuna ambao wanafikia umbali wa kuhoji kuwa ni kipengele hiki pekee ambacho kinaweza kuipa uhai kazi ya fasihi na kuifanya isimame kwenye maana halisi. Sikiliza hapa mhadhara wa Profesa Kulikoyela Kahigi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mbele ya Kongamano la 29 la Kiswahili la Bayreuth, kusini mwa Ujerumani. Continue reading “Sitiari katika kazi za fasihi”