Jitihada za ukusanyaji na uchambuzi wa data za kifoklo za launi za Kipemba si jambo geni (angalia Whiteley (1958) na Mlacha (1995:21-25). Lakini kadri, muda unavyopita jitihada hizo zinaelekea kupungua kasi. Suala la uhifadhi wa ‘bohari la hekima ya wahenga wetu kimaandishi’ ni la wajibu na halipaswi kusita. Katika mradi huu unaoendelea, tumeonelea kufanya mambo mawili makuu (a) kuorodhesha na kujadili data za kifoklo zenye kuweka wazi umahususi wa launi za Kipemba. (b) Kuorodhesha na kuchambua kiethnografia data hizo kwa mujibu wa mtazamo wa uchambuzi wa data za kifoklo kimuktadha (Hymes (1962).
Makala ya Ahmad Kipacha na Ibun Kombo wa Chuo Kikuu cha Dodoma iliyochapishwa kwa mara ya kwanza na Journal of Humanities, Toleo Na. 1 la mwaka 2009. Continue reading “Dunia kokwa ya furu: Amali ya Misemo ya KiPemba”