Sir James Mancham alikuwa rais wa kwanza wakati Seychelles inapata uhuru wake mwaka 1976, lakini akapinduliwa mwaka mmoja tu baada ya kuingia madarakani katika mapinduzi ambayo mwenyewe anaituhumu Tanzania kuhusika. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za kitabu alichokiandika mwanadiplomasia huyo wa kimataifa kuelezea maisha yake: Seychelles Global Citizen.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Seychelles Global Citizen cha Sir James Mancham”Tag: Ismail Jussa
TUFUNUWE KITABU: Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha
Sheikh Thabit Kombo Jecha ni miongoni mwa wazee wa Kizanzibari walioshiriki kikamilifu katika siasa za kabla na baada ya uhuru na mapinduzi visiwani Zanzibar akishikilia nafasi mbalimbali ndani ya chama cha Afro-Shiraz Party na baadaye CCM na pia kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ismail Jussa anatupitisha leo kwenye kurasa za simulizi za Sheikh Thabit kwa mujibu wa zilivyoandikwa na Kanali Hosana Mdundo wa Jeshi la Wananchi la Tanzania.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha”TUFUNUWE KITABU: Sowing the Wind cha Maulid Mshangama
Bwana Maulid Mshangama Haji aliajiriwa katika Utumishi wa Serikali mara aliporejea kutoka masomoni Makerere na akajikuta katika msukosuko baada ya kupingana na Kamishna Mkuu wa Utawala miongoni mwa Maofisa wa Kikoloni wa Kiingereza Zanzibar. Raghba za ujananchi zilimpelekea kuingia kwenye siasa akiunga mkono chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) na akawa mmoja miongoni mwa mawaziri vijana kwenye serikali ya mwanzo iliyokuja kupinduliwa Januari 1964. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za kitabu chake “Sowing the Wind: Zanzibar and Pemba Before the Revolution.”
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Sowing the Wind cha Maulid Mshangama”TUFUNUWE KITABU: Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar cha Hashil Seif
Katika mfululizo ya maandishi yaliyoandikwa juu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964, leo Ismail Jussa anatufunulia kurasa za kitabu cha Komredi Hashil Seif Hashil kinachosimulia maisha yake binafsi na ushiriki wake na chama chame cha Umma kwenye tukio hilo lililoibadilisha kabisa Zanzibar.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar cha Hashil Seif”