KISWAHILI KINA WENYEWE

Machozi Yamenishiya: Msafiri Safarini

MSHAIRI NA DIWANI YAKE

Linapokuja suala la kutaja mafanikio ya mshairi fulani, inatubidi kwanza tulikabili suala gumu la ki-ontolojia: ‘shairi ni nini’? Kwa vile suala hili hukosa jibu mwafaka, mimi hulipa fasili rahisi tu – yaani shairi ni umbo la sanaa-lugha linalojitofautisha na maumbo mengine ya sanaa-lugha kwa jinsi linavyosikika likisomwa kimoyomoyo au kinywa kipana. Shairi kwa hivyo, huvutia kwa utamu wake kimasikizi au kimaandishi kwa namna maneno ya kawaida yalivyoteuliwa na kupangwa kujenga hisia na kutoa taathira ya kiujumi na ujumbe. Continue reading “Machozi Yamenishiya: Msafiri Safarini”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Washindi wa tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya fasihi ya Kiafrika watangazwa

 

Tuzo ya Kiswahili ya Mabati Cornell ya Fasihi ya Kiafrika ilianzishwa na Prof. Mukoma Wa Ngugi na Dk. Lizzy Attree mwaka wa 2014 ili kuendeleza uandishi bora kwa lugha za Kiafrika na kuhimiza tafsiri kutoka lugha za Kiafrika kwa lugha nyingine, pia baina ya lugha za Kiafrika zenyewe kwa zenyewe. Continue reading “Washindi wa tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya fasihi ya Kiafrika watangazwa”