Nina furaha ya kumualika kwenye MSHAIRIKASTI mshairi kijana na mwenye kipaji wa Kiswahili kutoka Tanzania, Bashiru Abdallah, ambaye amechapisha diwani yake ya pili iitwayo Wino wa Dhahabu.
Tag: fasihi
Mwenye Wenyewe
Ni yeye mwenye wenyewe, mwenye asili na kwao
Ni yeye huyu ambaye, amebeba dira yao
Ndiye kwao alo yeye, na yeye kwake ni wao
TUPO: Diwani ya Tungo Twiti
Naamini kuwa hii ni kazi ya kwanza ya tungo ya mashairi ya Kiswahili kuandikwa katika ukamilifu wa kitabu kupitia mkusanyiko uliotokana na kuandikwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter. Na kama ndivyo basi roho na moyo wangu ni burdan kwa kuwa mtangulizi katika hili. Continue reading “TUPO: Diwani ya Tungo Twiti”
Kilio cha Usumbufu: Diwani mpya ya Kiswahili inayoangazia majanga ya kijamii
Ikiwa ni vigumu kusema kwa kinywa kipana ushairi ni nini, si vigumu kamwe kulitambua shairi zuri ni lipi. Mara unapolikabli (au tuseme linapokukabili), hukuvaa kwa nguvu za ajabu na kukupenya kwa hisia ya raha isiyoweza kuelezeka. Continue reading “Kilio cha Usumbufu: Diwani mpya ya Kiswahili inayoangazia majanga ya kijamii”