KISWAHILI KINA WENYEWE

Changi N’Kuchangizana: Tungo za Kiswahili

Ushairi ni sauti ya ndani. Ndani kabisa huko moyoni na huko kwenye chumba cha ndani cha ubongo, ambako mshairi hujisemesha na kuusemesha ulimwengu wake na wa wenzake. Ushairi ni hisia na pia ni fikira ya ndani. Kwa kuwa kwake sauti ya ndani, kunaufanya uwe kielelezo cha fikra huru za mwanaadamu, kwani huwa anajisemesha akiwa peke yake, pasina na nguvu za nje anazozikhofia kumsakamiza matambara mdomoni. Continue reading “Changi N’Kuchangizana: Tungo za Kiswahili”