UCHAMBUZI

Bila ya nguvu za dola na vurugu, CCM wepesi

Naandika makala hii refu baada ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, kujitokeza wiki mbii zilizopita kuwaasa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hasa wenyekiti Freeman Mbowe na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, kwamba wachunge kauli zao maana zinaweza kuwaweka pabaya kwa vile zina muelekeo wa kuvunja amani. Amani na utulivu ni misamiati ya kijanja inayotumika na Chama cha Mapinduzi (CCM) na mawakala wake kujijengea taswira kwamba wao ni watu wastaarabu, ilhali ni kinyume chake. Naamini naye DCI Manumba amezungumza zaidi kisiasa kuliko ‘kiulinzi’. Continue reading “Bila ya nguvu za dola na vurugu, CCM wepesi”