KISWAHILI KINA WENYEWE

TUPO: Diwani ya Tungo Twiti

Naamini kuwa hii ni kazi ya kwanza ya tungo ya mashairi ya Kiswahili kuandikwa katika ukamilifu wa kitabu kupitia mkusanyiko uliotokana na kuandikwa katika mtandao wa kijamii wa Twitter. Na kama ndivyo basi roho na moyo wangu ni burdan kwa kuwa mtangulizi katika hili. Continue reading “TUPO: Diwani ya Tungo Twiti”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Kalamu ya Ally Saleh kwenye ‘La Kuvunda’

Uandishi wa hadithi fupi unafanana na uandishi wa ushairi. Mote muwili, mwandishi hulieleza jambo kubwa na zito kwa maneno machache. Bila ya shaka hadithi fupi ni refu sana kuliko shairi, lakini ni fupi sana kuliko riwaya au hata novela. Mshairi hutafautiana na mwandishi wa hadithi fupi kwenye matumizi ya lugha, mapigo ya sauti na muziki wa ndani. Kwenye mawili yote hayo, Ally Saleh si mwepesi. Ameandika tungo kadhaa za ushairi kama ambavyo ameandika hadithi kadhaa fupifupi. Msome hapa kwenye mkusanyiko huu wa La Kuvunda. Continue reading “Kalamu ya Ally Saleh kwenye ‘La Kuvunda’”