NJOO uniulize Mohammed Khelef Ghassani ni nani na nitakupa vitambulisho vyake kadhaa. Kila kimoja kati yavyo kitamsibu. Kitajaa kama pishi. Continue reading “Mfalme Yuko Uchi: Diwani Mpya ya Mohammed Ghassani”
Tag: afrika mashariki
Wapi neno mwanana hutumika?

Juza, juvya, na julisha

Neno “juvya” si ‘athari ya matamshi tu’ bali ni mbadala wa “juza” na “julisha.” Liko katika lahaja ya Kimvita ( na latumika mpaka hivi leo), na nafikiri liko katika Kipemba na Kimtang’ata pia.
Ni “tanzia” au “taazia”?
Chembelecho (au chambilecho, au chambacho) msemo wa Kiswahili, “Kipya kinyemi, kingawa kidonda.” Ni dasturi ya baadhi ya watu kuvutiwa na kipya kitokacho kwengine, hata kama tangu hapo wanacho chao wenyewe kifananacho na hicho cha kigeni. Hili swala la maneno kama “mubashara” lina tanzu mbili. Utanzu wa kwanza ni huo wa kupenda kukimbilia maneno ya kigeni, hata kama tunayo yetu wenyewe yenye maana hiyo hiyo. Kama ilivyokwisha elezwa, kabla ya habari “mubashara” tumekuwa tukisema habari/ ripoti za moja kwa moja, au za papo kwa papo (wala si “papo” pekee).