KISWAHILI KINA WENYEWE

Kuhusu Mwanamajumui

Kabla ya kuelezaa maana ya neno “mwanamajumui”, kuna mambo mawili ambayo ni muhimu kuyaeleza. La kwanza, ni kwamba kuna wasemao “mwanaumajumui”; na baadhi ya watu huidondosha hiyo u walitumiapo neno hilo. Continue reading “Kuhusu Mwanamajumui”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Baina ya mkandarasi na kandarasi – 2

Nimetangulia kusema kwamba hayo niliyoyaeleza kabla hayakuwa yamenishughulisha sana kwa sababu, mtu aweza kuwa na hiari ya kutumia maneno kandarasi/makandarasi au mkandarasi/wakandarasi, akusudiapo kuwa ni mtu. (Mimi nitaendelea kutumia kandarasi/makandarasi – tena bila ya wasiwasi wowote!) Continue reading “Baina ya mkandarasi na kandarasi – 2”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Baina ya mkandarasi na kandarasi – 1

contractorsafety_img_4433Mmojawapo miongoni mwa washairi maarufu wa Tanzania, Khamis Amani Nyamaume (1926-1971), katika shairi lake labeti nne, liitwalo ‘Saa’, alitunga akasema:

Saa za huku na huko, zimekosana majira
Sababu ni mzunguko, haufuati duara
Sasa rai iliyoko, ni kubadilisha dira
Saa zatupa majira, mafundi zitengezeni… Continue reading “Baina ya mkandarasi na kandarasi – 1”