UCHAMBUZI

Nguvu ya Lissu ni kubwa kuliko ya risasi

Sisi wengine tangu siku ya mwanzo akina Nape Nnauye walipokuwa wakitetea uamuzi wa serikali ya awamu ya tano kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge kupitia televisheni ya taifa kwa madai ya kubana matumizi, tulijuwa wameshachelewa. Continue reading “Nguvu ya Lissu ni kubwa kuliko ya risasi”

UCHAMBUZI

Lissu wa dhahabu

Mkononi mwangu nina kitabu kiitwacho ‘A Golden Opportunity? Justice & Respect in Mining’ (Fursa ya Dhahabu? Haki na Heshima kwenye Madini) cha mwaka 2008. Waandishi wake ni wawili – Mark Curtis na Tundu Lissu. Ni matokeo ya utafiti uliofanywa na wawili hao wakiwa chini ya Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na uchapishaji wake kufadhiliwa na Shirika la Misaada la Kikristo la Norway. Continue reading “Lissu wa dhahabu”

UCHAMBUZI

Maisha yasiyotathminiwa hayana maana kuyaishi

Ulimwenguni kote na katika zama zote, jamii inapokuwa chini ya utawala ulioziba masikio na macho na nyoyo, watawala hupenda waachiwe wafanye watakavyo. Huwa wamejirithisha wenyewe nchi na raia wake. Na kwa hili hawataki muhali, masahihisho, wala mabadiliko. Anapotokea mtu kuwasahihisha, badala ya kumchukulia kuwa msaidizi, wao humchukulia adui wao nambari moja, na hivyo hujihalalishia kumuadhibu kwa namna yoyote waionayo inafaa. Continue reading “Maisha yasiyotathminiwa hayana maana kuyaishi”

UCHAMBUZI

Taifa lisilowaomboleza wahanga wake, haliwezi kuwaadhimisha mashujaa wake

Usiku wa kuamkia tarehe 10 Septemba 2011, meli ya Mv Spice Islander iliondoka kisiwani Unguja kuelekea Pemba ikiwa imejaza kupita uwezo wake halisi. Inasemekana kuwa ndani yake mulikuwa na abiria zaidi ya 3,000 badala ya 645 iliotakiwa kisheria. Ilikuwa pia na shehena kubwa ya mizigo. Continue reading “Taifa lisilowaomboleza wahanga wake, haliwezi kuwaadhimisha mashujaa wake”