BLOG POSTS, UCHAMBUZI

Iwache jamii iihukumu sanaa

Mimi si mtu wa huu uitwao muziki wa kizazi kipya kwa sababu nina matatizo ya kimsingi na ufasihi wa fasihi iliyomo ndani yake na pia ufinyu na mawanda ya neno SANAA panapohusika kazi zao. Lakini nawatambua waufanyao muziki huu na nawahishimu kwa kazi yao.

Continue reading “Iwache jamii iihukumu sanaa”
UCHAMBUZI

Taazia: Kwaheri Maalim Suleiman Shkeli wa Pandani

Mauti ewe mauti, ukija kama hujaja
Huwa waja katikati, ya maisha yetu waja
Katikati ya wakati, na kati ya zetu haja
Na hata tukikutaja, wewe khabari hupati

Nimepokea habari ya Kaka yangu, Mzee wangu, Muhisani wangu, Sheikh Sulaiman Al Shukaili, kuitikia wito wa Aitaye akalazimika kuitikwa. Asubuhi hii karudi kwa Mola wake. Allah Ampokee ilhali keshamsamehe makosa yake na aifanye pepo iwe nyumba yake. Amin Yaa Rabb. Continue reading “Taazia: Kwaheri Maalim Suleiman Shkeli wa Pandani”

UCHAMBUZI

Mayatima na wajane wa kisiasa hadi lini Zanzibar?

Ali Juma Suleiman alivamiwa na kikosi kikubwa cha watu usiku wa tarehe 26 Septemba mwaka huu nyumbani kwake Mtoni, Unguja. Mke wake, Bi Rehema Nassor Juma, anasema alishuhudia askari wenye sare za vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakiwa na mitutu ya bunduki, marungu na mapanga. Continue reading “Mayatima na wajane wa kisiasa hadi lini Zanzibar?”