BLOG POSTS, UCHAMBUZI

Ninaishi Magharibi

Kwa lugha na utamaduni wangu, magharibi ina maana nyingi: ndiko jua linakotulia likaibadilisha leo kuwa jana na kuitayarisha kesho kuwa leo. Ndicho kielelezo pia cha kumalizika kwa maisha ya mwanaadamu ya hapa duniani, maana magharibi kawaida huja na giza, na giza ni alama ya mauti. Magharibi pia ni nadharia ya kisiasa kwenye medani za kilimwengu na lugha yangu imeipokea hivyo hivyo – kuwa ni mataifa ya Ulaya na Marekani yanayoambiwa yameendelea kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Continue reading “Ninaishi Magharibi”
BLOG POSTS, UCHAMBUZI

Uhusiano baina ya ukosefu wa demokrasia na kushamiri kwa ufisadi

Uchambuzi huu unakusudia kuonesha – kwa nadharia – uhusiano mkubwa uliopo baina ya ukosefu wa demokrasia na kushamiri kwa ufisadi. Hoja ni kwamba kadiri demokrasia inavyokosekana ndivyo ufisadi unavyojiimarisha na kisha nao ufisadi ukazuwia demokrasia kufanya kazi yake.

Continue reading “Uhusiano baina ya ukosefu wa demokrasia na kushamiri kwa ufisadi”