Ni mkubwa mtihani, alouzusha nguruwe
Aliye asi zizini, yeye na maswahibuwe
Kuingiza ufitini, watakalo lao liwe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi? Continue reading “Nimtoweje zizini?”
Category: KISWAHILI KINA WENYEWE
Sarufi, Fasihi, Ushairi, Uchambuzi wa Lugha ya Kiswahili
Tafrani: Tamthiliya ya Vita Baina ya Ukale na Usasa
Jamii ya Kizanzibari inapitia kwenye vipindi vyake vya mabadiliko kama zilivyo jamii nyengine zozote za kibinaadamu. Kubadilika kwa jamii huwa ni sehemu muhimu ya maisha na, kwa hakika, si adui wa maisha ya mwanaadamu. Continue reading “Tafrani: Tamthiliya ya Vita Baina ya Ukale na Usasa”
Kalamu ya Ally Saleh kwenye ‘La Kuvunda’
Uandishi wa hadithi fupi unafanana na uandishi wa ushairi. Mote muwili, mwandishi hulieleza jambo kubwa na zito kwa maneno machache. Bila ya shaka hadithi fupi ni refu sana kuliko shairi, lakini ni fupi sana kuliko riwaya au hata novela. Mshairi hutafautiana na mwandishi wa hadithi fupi kwenye matumizi ya lugha, mapigo ya sauti na muziki wa ndani. Kwenye mawili yote hayo, Ally Saleh si mwepesi. Ameandika tungo kadhaa za ushairi kama ambavyo ameandika hadithi kadhaa fupifupi. Msome hapa kwenye mkusanyiko huu wa La Kuvunda. Continue reading “Kalamu ya Ally Saleh kwenye ‘La Kuvunda’”
Kubana Matumizi ni Kupi?
Wakale kenda safari kwa ndege, usukani marubani wawili
Mwengine leo hii vyereje, kwa msururu wa gari?
Njiani kihanikiza vishindo na shangwe, keli ya kubana hali
Ninaomba nielezwe, kubana matumizi ni nini? Continue reading “Kubana Matumizi ni Kupi?”