
Wapi neno mwanana hutumika?

Poet. Multimedia Journalist. Author
Chembelecho (au chambilecho, au chambacho) msemo wa Kiswahili, “Kipya kinyemi, kingawa kidonda.” Ni dasturi ya baadhi ya watu kuvutiwa na kipya kitokacho kwengine, hata kama tangu hapo wanacho chao wenyewe kifananacho na hicho cha kigeni. Hili swala la maneno kama “mubashara” lina tanzu mbili. Utanzu wa kwanza ni huo wa kupenda kukimbilia maneno ya kigeni, hata kama tunayo yetu wenyewe yenye maana hiyo hiyo. Kama ilivyokwisha elezwa, kabla ya habari “mubashara” tumekuwa tukisema habari/ ripoti za moja kwa moja, au za papo kwa papo (wala si “papo” pekee).
Kwa uchache wa nifahamuvyo, lugha fasaha ni kusema “kiasi cha…”, basi haidhuru iwe ni kwa watu au kwa vitu. Yaani, kiasi cha watu kumi, au kiasi cha miti kumi. Kama ambavyo twasema, kitabu cha…, kisa cha…, kiatu cha…, kitambo cha…, na kadhalika, wala hatusemi kitabu ya…, kisa ya…, kiatu ya…, wala kitambo ya… Na ni hivyo kwa sababu maneno yote hayo yamo katika ngeli ya KI/VI. Basi ikiwa kwa maneno hayo niliyoyatolea mfano hatuyatumilii “ya”, kwa nini iwe kwa neno “kiasi”?