KISWAHILI KINA WENYEWE

Kilio cha Usumbufu: Diwani mpya ya Kiswahili inayoangazia majanga ya kijamii

Ikiwa ni vigumu kusema kwa kinywa kipana ushairi ni nini, si vigumu kamwe kulitambua shairi zuri ni lipi. Mara unapolikabli (au tuseme linapokukabili), hukuvaa kwa nguvu za ajabu na kukupenya kwa hisia ya raha isiyoweza kuelezeka. Continue reading “Kilio cha Usumbufu: Diwani mpya ya Kiswahili inayoangazia majanga ya kijamii”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Maana nne za “Likikupata, patana nalo”

Karibuni nilikuwa kwenye ziara kwenye mataifa mawili ya Kiarabu – Oman iliyo Ghuba na Morocco iliyo Afrika Kaskazini – ambayo yana tafauti nyingi baina yao, lakini pia yana mfanano mkubwa kwenye mtazamo wao kuelekea lugha ya Kiarabu. Watu wa mataifa yote mawili watakuambia sentensi moja inayofanana: “Kiarabu ni lugha kongwe na ya kihisabati!” Continue reading “Maana nne za “Likikupata, patana nalo””

KISWAHILI KINA WENYEWE

Baina ya mkandarasi na kandarasi – 2

Nimetangulia kusema kwamba hayo niliyoyaeleza kabla hayakuwa yamenishughulisha sana kwa sababu, mtu aweza kuwa na hiari ya kutumia maneno kandarasi/makandarasi au mkandarasi/wakandarasi, akusudiapo kuwa ni mtu. (Mimi nitaendelea kutumia kandarasi/makandarasi – tena bila ya wasiwasi wowote!) Continue reading “Baina ya mkandarasi na kandarasi – 2”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Baina ya mkandarasi na kandarasi – 1

contractorsafety_img_4433Mmojawapo miongoni mwa washairi maarufu wa Tanzania, Khamis Amani Nyamaume (1926-1971), katika shairi lake labeti nne, liitwalo ‘Saa’, alitunga akasema:

Saa za huku na huko, zimekosana majira
Sababu ni mzunguko, haufuati duara
Sasa rai iliyoko, ni kubadilisha dira
Saa zatupa majira, mafundi zitengezeni… Continue reading “Baina ya mkandarasi na kandarasi – 1”