KISWAHILI KINA WENYEWE

Kiswahili kina wenyewe, kienee lakini kisitokomee

Utangulizi

Kama zilivyo lugha nyingi zilizopata bahati ya kuwa kiunganisho baina ya wazungumzaji kutoka makabila na mataifa mengine, Kiswahili nacho kina wenyewe wenye asili nacho na kina watumiaji wa kawaida. Continue reading “Kiswahili kina wenyewe, kienee lakini kisitokomee”

KISWAHILI KINA WENYEWE

Sahihi ni Ipi: Sala au Swala?

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

رَبِّ اشْرَحْ لِي صَدْرِي ﴿٢٥﴾ وَيَسِّرْ لِي أَمْرِي ﴿٢٦﴾ وَاحْلُلْ عُقْدَةً مِّن لِّسَانِي ﴿٢٧﴾ يَفْقَهُوا قَوْلِي

Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu, Na unifanyie nyepesi kazi yangu, Na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, Wapate kufahamu maneno yangu. (Suratu Maryam Aya ya 25-28)

UTANGULIZI

Mimi si mtaalamu wa lugha, wala si mweledi katika uandishi. Sikuondokea kujishughulisha na kazi ya uandishi, na bahati mbaya mpaka sasa nimebaki vivyo hivyo. Japokuwa sina ufasaha pia katika uzungumzaji, lakini huwa ninafadhilisha kufikisha makusudio yangu kwa njia ya uzungumzaji kuliko uandishi. Kwa sababu hiyo, nimekuwa nikitembea nalo kichwani mwangu kwa muda mrefu, dukuduku langu la haya nitakayoyaeleza katika andiko hili, mpaka hivi karibuni ilipotokea sababu ya heri iliyonipa msukumo wa kukaa kitako na kuchapa maneno haya. Continue reading “Sahihi ni Ipi: Sala au Swala?”