JAMII za Waswahili daima zimekuwa na mihimili inayoshikilia silka na tamaduni zake. Zimekuwa na taasisi imara za ujenzi na uendelezaji wa maisha, mitazamo, falsafa na imani zao. Kuanzia chini kabisa hadi juu kabisa, maisha ya watu wa Uswahilini huwa si matupu. Kila ombwe hujazwa kwa tanzu, bahari na mikondo ya sanaa na usanii, fasihi na ufasaha.
Continue reading “SIMULIZI ZA BI TIME: Hadithi za Ncha Saba”Category: KISWAHILI KINA WENYEWE
Sarufi, Fasihi, Ushairi, Uchambuzi wa Lugha ya Kiswahili
Baina ya Mkosaji, Mkoseaji na Mkosefu
Mkosaji, mkoseaji na mkosefu ni watu watatu tafauti kwa Kiswahili, ingawa kuna mahala panaweza kuwa na mgusano wa kimantiki.
Continue reading “Baina ya Mkosaji, Mkoseaji na Mkosefu”Mfalme Yuko Uchi: Diwani Mpya ya Mohammed Ghassani
NJOO uniulize Mohammed Khelef Ghassani ni nani na nitakupa vitambulisho vyake kadhaa. Kila kimoja kati yavyo kitamsibu. Kitajaa kama pishi. Continue reading “Mfalme Yuko Uchi: Diwani Mpya ya Mohammed Ghassani”
Kuhusu Mwanamajumui
Kabla ya kuelezaa maana ya neno “mwanamajumui”, kuna mambo mawili ambayo ni muhimu kuyaeleza. La kwanza, ni kwamba kuna wasemao “mwanaumajumui”; na baadhi ya watu huidondosha hiyo u walitumiapo neno hilo. Continue reading “Kuhusu Mwanamajumui”