Wakati Ulimwengu wa Kiislamu ukikumbuka miaka 100 tangu kutawafu kwa ulamaa mkubwa wa Afrika Mashariki na Bahari nzima ya Hindi, Habib Ahmad bin Sumeit, Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za kitabu kiitwacho “Sufis and Scholars of the Sea” kilichoandikwa na mtafiti maarufu wa Norway, Profesa Anne Bang, kinachoangazia maisha na nyakati za mwanazuoni huyo mkubwa kabisa wa zama zake na pia safari na maingiliano ya watu kupitia Bahari ya Hindi yalivyochangia kueneza elimu ya dini ya Kiislamu katika miji ya Mwambao wa Afrika Mashariki kwa karne nyingi.
Continue reading “Maisha na Nyakati za Habib Ahmad bin Sumeit kupitia ‘Sufis and Scholars of the Sea’ cha Anne Bang”Category: BLOG POSTS
TUFUNUWE KITABU: Gone With the Tide cha Fatma Jinja
Bi Fatma Jinja aliyaishi maisha yake akipitia milima na mabonde na sehemu kubwa ya namna alivyokabiliana nayo haikuwahi kufahamika na waliokuwa kando yake ambao, badala yake, waliyatafsiri makabiliano hayo kwa wapendavyo wenyewe. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za moja kati ya vitabu vyake vitano, Gone With the Tide, kinachosimulia hadithi ya maisha yake.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Gone With the Tide cha Fatma Jinja”TUFUNUWE KITABU: Zanzibar: The Last Years of the Protectorate
Leo, ismail Jussa anachambuwa jinsi Bwana Maulid Mshangama kupitia kitabu chake “Zanzibar: The Last Years of the Protectorate” anavyotowa ushahidi wa kina wa namna utawala wa Waingereza ulivyopanga vitimbi na hila za makusudi dhidi ya Zanzibar kuhakikisha kuwa visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi kamwe havisimami kama taifa huru linalojitegemea.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Zanzibar: The Last Years of the Protectorate”TUFUNUWE KITABU: Seychelles Global Citizen cha Sir James Mancham
Sir James Mancham alikuwa rais wa kwanza wakati Seychelles inapata uhuru wake mwaka 1976, lakini akapinduliwa mwaka mmoja tu baada ya kuingia madarakani katika mapinduzi ambayo mwenyewe anaituhumu Tanzania kuhusika. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kurasa za kitabu alichokiandika mwanadiplomasia huyo wa kimataifa kuelezea maisha yake: Seychelles Global Citizen.
Continue reading “TUFUNUWE KITABU: Seychelles Global Citizen cha Sir James Mancham”