Wakati Zanzibar inapata uhuru wake uliodumu kwa mwezi mmoja kabla ya kupinduliwa na kisha kuunganishwa na Tanganyika kulikoifanya iwe sehemu ya dola la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwanadiplomasia wa Kimarekani, Don Petterson, alikuwa kwenye mwanzoni mwa kazi zake za kibalozi nchini Zanzibar. Kupitia kurasa za kitabu hiki, anazungumza alichokishuhudia na alivyokifahamu kwa mtazamo wa Kimarekani.