Sheikh Thabit Kombo Jecha ni miongoni mwa wazee wa Kizanzibari walioshiriki kikamilifu katika siasa za kabla na baada ya uhuru na mapinduzi visiwani Zanzibar akishikilia nafasi mbalimbali ndani ya chama cha Afro-Shiraz Party na baadaye CCM na pia kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Ismail Jussa anatupitisha leo kwenye kurasa za simulizi za Sheikh Thabit kwa mujibu wa zilivyoandikwa na Kanali Hosana Mdundo wa Jeshi la Wananchi la Tanzania.