Profesa Abdulrahman Mohamed Babu alikuwa mmoja kati ya wanasiasa mashuhuri wa Zanzibar, ambao fikra zake ziliwaathiri wanasiasa wengi wakubwa na wadogo wa zama zake lakini – kama ilivyo kwa wanasiasa wengine wa aina yake – si mengi yanayofahamika miongoni mwa vijana wa sasa kumuhusu. Ismail Jussa anatupitisha kwenye kitabu cha ‘Babu: I Saw the Future and It Works’ kilichohaririwa na Marehemu Profesa Haroub Othman kikikusanya maandishi ya mwenyewe Profesa Babu na wasomi wengine.