Kwenye mfululizo mpya wa LULU ZA ZANZIBAR, ambao unakusudia kuwasaka Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi yao na waliofika hatua kubwa katika taaluma ama kazi zao, tunaanza na Profesa Abdulaziz Yussuf Lodhi, mzaliwa wa Mkunazini, Mji Mkongwe, kisiwani Unguja, ambaye kwa sasa ni mstaafu anayeishi nchini Sweden.