
Nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikiwasikia wazee wakiitumia sifa hiyo, -anana, kwa vitu vinavyohisika, vinavyodirikika, au vinavyoonekana kwa akili au kwa hisia. Kwa mfano, upepo mwanana (upepo unaopuliza kwa upole na utulivu); sauti nyanana (sauti nzuri inayopendeza masikioni na kuburudisha); ngozi nyanana (ngozi nyororo); maji manana (maji yaliyotuwama au kutiririka kwa upole); mtu mwanana (mtu mpole, mwenye tabia nzuri na maingiliano mazuri na wenziwe).
Ni katika utuuzimani mwangu ndipo nilipoisikia sifa hiyo ikitumiliwa karibu kila kitu. Ndipo tukawa twasikia, au kusoma, nyumba nyanana, gari lanana, na kadhalika.
Hayo ndiyo niwezayo kuyaeleza kwa ufupi.
Twanufaika mwalimu. Endelea kutufunza, Mngu akupe uzima, hekima na busara zaidi. Amin
wanatia hamasa wa kuandika vitabu katika lugha ya kiswahili, ubarikiwe mwalimu