KISWAHILI KINA WENYEWE

Nimtoweje zizini?

Ni mkubwa mtihani, alouzusha nguruwe
Aliye asi zizini, yeye na maswahibuwe
Kuingiza ufitini, watakalo lao liwe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi?

Niwakumbushe mwanzoni, walimwengu muelewe
Alikimbia zizini, na sababu asitowe
Katuacha mkondoni, mawimbi yatupinduwe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi?

Akaitisha mitingi, manyani na hata mwewe
Wazo lake la msingi, mbele yao atongowe
Zizini ‘mezuka gengi, ahofia uhaiwe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi?

Leo karudi zizini, kuupima ulimiwe
Ameuweka mezani, angoja ahukumiwe
Watu mate vifuani, wataka waununuwe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi?

Atikisa kichwa chake, atekenywapo nguruwe
Ili bwana aridhike, aendesha mtajiwe
Anaonesha makeke, wengine tusulubiwe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi?

Ana ulinzi mkali, kuulinda umuriwe
Watu walo vimba mili, wanamlinda nguruwe
Mabomu ya pilipili, sio marungu na mawe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi?

Ila yupo kitanzini, namueleza ajuwe
Ataondoka zizini, watu wasisumbuliwe
Atokomee porini, huko asahauliwe
Nimtoweje zizini, guruwe aliyeasi?

Nimefika kituoni, mikono niinyanyuwe
Haki irudi mezani, watu wasidhulumiwe
Mukangia kufuruni, kisa kesi ya nguruwe
Nimtoweje zizini, nguruwe aliyeasi?

@Mahmoud.S Juma
07 Septemba 2016

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.