Kumekuwa na mjadala mrefu miongoni mwa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ikiwa kile kichachoitwa Kiswahili Sanifu ni lugha kamili na tafauti na lugha nyengine zinazozungumzwa kwenye maeneo yanayopakana nacho, kama vile Kimakunduchi (au Kikaye) kinachozungumzwa kusini mwa kisiwa cha Unguja, au zote kwa pamoja ni lahaja za lugha moja kuu, yaani Kiswahili. Msikilize Dk. Hans Mussa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichambua tafauti baina ya Kimakunduchi na Kiswahili Sanifu mbele ya hadhara ya Kongamano la 29 la Kiswahili la Bayreuth, kusini mwa Ujerumani.
https://soundcloud.com/mohammed-k-ghassani/tafauti-baina-ya-kimakunduchi-na-kiswahili-sanifu