KISWAHILI KINA WENYEWE

Lata na Ng’uza

‘Mengia Lata na N’guza, wakidai wao Mungu
Nasi bila kuchunguza, tukavaa zao pingu
Sasa wanatutatiza, kwa idhara na virungu

 • Miujiza walisema, tutaiona haraka
  Wagonjwa wangesimama, na wafu wangefufuka

  Nyati angekuwa kima, na simba akawa paka

   

  Edai neema Lata, majumbani zitajaa
  Shida tutaitafuta, na raha zitatuvaa

  Yote hatukuyapata, labda nyingi balaa

   

  Simba amekuwa paka, na paka hajulikani
  Nyati kageuka nyoka, atambaa majanini

  Kima juu anashuka, ataka kazi za ndani

   

  Bata amekuwa chui, na ng’ombe kawa pelele
  Kuku hawafi kwa ndui, wamalizwa na uzile

  Na mdudu buibui, ala shina na viale

   

  N’guza ataka tutii, kwa kadiri apendavyo
  Lakini hayajutii, mambo yetu Kenda ovyo

  Wanyonge hasaidii, wanabaki hivyo hivyo

   

  Kwa nguvu Lata adai, tumpe sijida zetu
  Anasema hawajui, Mola na Mtume wetu

  Lakini hayaondoi, mabaya yalofurutu

   

  N’guza yeye atunyima, tusile ashibe yeye
  Atesa hata wanyama, hajali hata nduguye

  ‘Kimhoji utamkoma, kusema ukujutiye

   

  Lata adai na nguvu, ahuuwisha akifisha
  ‘Kisema ana ubavu, makubwa kuyadogosha

  Atia watu makovu, wanyonge aadabisha

   

  N’guza atwaa ya kwake, na yaliyomzunguka
  Vyote wiwe chini yake, tumuombe tukitaka

  Ni bahari tumbo lake, lazibeba hata taka

   

  Jichole lina mtoto, Lata haoni vizuri
  Japo mwembamba kya fito, vazi lake ni kiburi

  Kwa maneno ya mkato, Lata yeye ni tajiri

   

  N’guza japo anaona, rangi zote hazijui
  Kwake zote za fanana, nyeupe na baibui
  Kazi yake kutubana, vyetu vimo havikui
 •  

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.