KISWAHILI KINA WENYEWE

Watakani?

Hivi watakani?
Twambie..
Roho zetu, uzichukue?
Utu wetu, uuondoe?
Mali zetu, uzigawe?

Twambie basi..
Kama kula, u pekeyo..
Utakula shibeyo
Nyama kula upendayo..
Vipi bado watutesa?

Waingia kwetu usiku
Wavunja letu
Banda la kuku
Huku ukitikatika..
Amba buku..
Sisimizi wewe ajabu

Nyumbani wa hina hina
Kwa nini?
Wajifanya ja Mchina
Ukaratini
Waitaka fitina
‘Mebaini
Sisimizi u shidani

Watuona amba jiwe
La angani
Hutaki uangukiwe
Kisogoni
Kutwa unawasha wewe
Mwilini
Hutosheki?

Chakula ‘shapakua..
Wangojani?
Vipi si watunyukua?
Vitandani
Kisa twala halua
Yakuhusu ni??
Bure unajisumbua

Chakula chak0
Kimoto
Ila situmie kijiko
Kitakudanganya..

Amour Hadji
Zanzibar
31 Januari 2016

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.