Sili kattu miye sili, sili kilicho haramu, hali nakijuwa fika
Nakijuwa si halali, sili kilicho na sumu, nikila nitadhurika
Kingarembwa kwa asali, kionekane kitamu, na kawa kikafunikwa
Sikili kamwe sikili, kichwani mwangu timamu, nawale walopotoka!
Mohammed K. Ghassani kutoka Diwani ya Kalamu ya Mapinduzi
Safi kaka
Sent from my iPhone
>
Safi sana khelefu.