Mie kwanza kwa isimu
Kumzukuru karimu
Alie iumba damu
Mwilini katembea
Ni yeye mwenye uweza
Alo ipanua chaza
Kwenye mkondo wa kiza
Lulu kaibarikia
Nimshukuru rabana
Hazawa nami nmwana
Kwenye visiwa mwanana
Jinale zinjibaria
Huwaingia majonzi
Wapitao na jahazi
Hawana hata ushanzi
Katika vyetu visiwa
Nafsi zawatamani
Ijapo iwe zamani
Mababu arubaini
Apate pakuungia
Kwa kua nsifa nno
Sie kuzaliwa huno
Inakua ni nfano
Duniani watolewa
Azuke karibu nasi
Ajitie ukakasi
Atupake makamasi
Huku akiturandia
Ajioneshe nfano
Eti kan’zongwa nno
Apenda nshikamano
Mahaba yakumuua
Aupenda aung’ariza
Akilala auwaza
Asubuhi ang’aruza
Ungalipo au laa.
Aje atushupalie
Kwasifa atusifie
Kwa ghera asimamie
Tusiseme lilo sawa
Yumkini ntu huyu
Yumo akaanga mbuyu
Nwawapi bwana huyu
Mbona kutubururia?
Ikanishia tamaa
Haiwi awe jamaa
Akatuletea haaa
Huyu wakutumiliwa
Hikaa mepumbuwaa
Fikira zimenijaa
Nikashituli haaaaa!
Huyu si wakudandia
N’wetu wa mwilini
Kapotelea porini
Karudi kuja tukhini
Damuye ilomzaa
Huyu si wa kule nno
Mbali vidole vitano
Huhitaji malumbano
Atojapo wapajua
Nikajirudisha nyuma
Kupekura nlosoma
Nazinga ile heshima
Mbona inanipotea?
Nikaunga unga doti
Sikupata tofauti
Mwenye kuku kwenye koti
Kashaaza kumyea
Eeeeh mola mtenze nguvu
Usimpe ushupavu
Akatupaka utonvu
Urimboni kututia
Ishamwishia tamaa
Karudi kujikalia
Wale walomtumia
mbwembwe wanamtilia
Yarabi usimkhini
Na kuchi wake kotini
Ende nae kaburini
Siku atayo jifia.
Atoya
2015