Apendaye yuajali, hujali ampendaye
Sababu ndiye suali, na ndiye majawabuye
Ambwapo mpenzi hali, hujiona hali yeye
Mwenziwe ‘kiwa halali, hiyo huwa ni dhikiye
Kwa nahari na layali, huizinga sababuye
Hutaka kwa kulla hali, aione thamaniye
Ndipo yakambwa mapenzi!
Mohammed K. Ghassani
9 Januari 2016
Bonn