“Kiswahili kimeingiliwa” ndivyo wanavyoamini wahafidhina wa lugha hii – wale ambao wanaamini kuwa mabadiliko yoyote yanayoingia kwenye lugha yana athari na hatari ya moja kwa moja ya kupoteza uhalisia wa lugha yenyewe na hivyo uwezekano wa hata kukiua kabisa Kiswahili.
Kuingiliwa huku kwa Kiswahili sio tu kwenye matamshi na maneno, bali pia kwenye tanzu muhimu ya fasihi, ambayo kwa sasa inashuhudia kuibuka kwa kile kilichopewa jina la “Fasihi-Pendwa” au fasihi ya kisasa. Kwa namna gani fasihi hiyo inatafautiana na fasihi ya kale au kama wengine wanavyoiita “Fasihi Halisi”?
Fuatana na Dk. Aldin Mutembei wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hapa kujifunza mengi juu ya hayo, pamoja na kusikia juu ya nadharia mpya ya Korasi katika uchambuzi wa fasihi, nadharia ambayo imetungwa na mwenyewe Dk. Mutembei.